Maswali na Majibu Kuhusu Biashara ya Forex
Forex ni nini?
Forex ni ubadilishaji wa Fedha za kigeni yaani Foreign Exchange, na neno Forex, ni ufupisho wa maneno hayo yaani Foreign Exchange.
Kuna tofauti gani kati ya Forex ya mtandaoni na ile ya Bureau De Change au Banks?
Forex ya Bureau De Change au maduka ya kubadilishia Fedha za kigeni, au ile ya kwenye ma benk, inahusisha kubadilisha Fedha za kigeni zilizopo kwenye mfumo wa makaratasi yaani CASH, lakini Forex ya mtandaoni, inahusisha matumizi ya mtandao wa internet kuweza kufanya ubadilishano wa fedha za kigeni na ni huduma inayowezeshwa na mwezeshaji aliye katikati ambaye hufahamika kama Forex Broker.
Nini maana ya Broker kwenye Forex?
Forex Broker ni taasisi inayosimama katikati ya wafanyabiashara wa forex (Forex traders) na masoko ya Forex kwa kuwezesha kuuza na kununua fedha za kigeni.
Naweza ku-trade Forex muda wowote?
Biashara ya Forex, inawezeshwa na Forex brokers, ambao huwa wanatoa uwezo au access ya kuuza na kununua fedha za kigeni, pindi masoko ya kubadilisha fedha za kigeni yanapofunguliwa, Masoko haya hufanya kazi kwa muda wa kazi wa nchi husika, mara nyingi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni kwa masaa ya nchi husika, nchi hizo ambazo zina masoko ya kubadilisha fedha za kigeni ni Marekani ambayo ina masoko makuu mawili (New York Stock Exchange na NASDAQ), Uingereza ambayo ina soko la London Stock Exchange, Ujerumani, Japan, Australia na New Zealand. Masoko haya hufunguliwa kwa masaa tofauti tofauti kulingana na time zone ya nchi husika na hufungwa nyakati za weekend, yaani Jumamosi na Jumapili.
Je Forex ni utapeli kama biashara za Upatu?
Jibu jepesi ni HAPANA. Forex trading ni biashara halali kabisa na imekuwepo kwa miaka mingi na itaendelea kuwepo, na haina uhusiano wala haifanani na biashara za Upatu.
Je nahitaji elimu gani ku-trade Forex?
Huhitaji elimu yoyote maalum kuwa mfanya biashara mzuri wa Forex, ingawa ni faida zaidi kwako iwapo una elimu ya fedha (Financial Education).
Je nahitaji mtaji kiasi gani kuanza Forex?
Mtaji wa kuanza Forex unatofautiana kati ya broker na broker, wapo baadhi ya Broker ambao wanaruhusu kuanza na kiwango kidogo hata dola 5, kwa mfano XM.COM na hata kiwango cha chini kabisa cha dola 1 kwa mfano TemplerFX na wapo baadhi ya broker wengine ambao kianzio ni dola 200 za kimarekani, kwa mfano Pepperstone.
Je faida ya Forex inapatikana vipi?
Faida ya Forex inapatikana pale unapoenda uelekeo sahihi na uelekeo wa soko la forex kwa pair uliyoamua kuuza au kununua. Kwa mfano, kama umeamua kununua EURUSD, halafu sarafu ya EURO ikawa na nguvu kuliko USD, inamaanisha utakua ume BUY uelekeo sahihi, hii itapekekea wewe kupata faida pale utakapo funga position hiyo uliyofungua.
Nawezaje kujiunga na biashara ya Forex?
Kujiunga na biashara ya Forex, unahitaji kuamua kuchagua broker utakayemtumia, kwa mfano kama ukipenda kumtumia broker aitwaye TemplerFx, basi BOFYA HAPA kutengeneza account, kwa orodha ya brokers wengine, BOFYA HAPA. kusoma zaidi jinsi ya kujiunga na Forex, BOFYA HAPA