Support and Resistance
Hii ni moja kati ya strategy za awali kabisa katika forex na walimu wengi huwa wanaifundishaga but sisi wanafunzi wengi huwa tukishaanza kujua vitu vingine vya mbele kama trendline na vinginevyo basi huwa tunaipuuza hii strategy, ila kiuhalisia hii ndio strategy mama, nkisema strategy mama namaanisha strategy nyingi za forex zimeanzia hapa.
N.B:
Kama ndio unaanza kujifunza biashara ya Forex, unashauriwa kujiunga kwa kutengeneza account kwa broker anayekubalika zaidi Afrika Mashariki:
Ukishatengeneza account, hakikisha una verify email yako pamoja na namba yako ya simu.
Kwahiyo support na resistance ni muhimu kuijua na kuizingatia coz hii ndio imebeba forex na kuthibitisha hili embu tuongee kuhusu forex kuhusisha na hili.
Kwenye forex huwa kunaforce mbili ambazo ndio hasa zinafanya soko litembee juu au chini na wakati mwingine litulie sehemu moja.
Hizi force ni Demand na Supply
Demand hii ni force ambayo inasababisha price kutoka chini kupanda juu na demand ndio huwa tunawaita buyer yani wanunuzi.
Supply hii nayo ni force ambayo inachukua price kutoka juu nakuishusha chini kuelekea kwa demand na supply kwa maana nyingine ni seller yani wauzaji.
Kwahiyo endapo demand watakua na nguvu kuliko supply basi hapa ndio tunaona soko linamove kutoka chini kwenda juu na endapo supply watakua na nguvu kuliko demand basi hapa ndio tunaona soko linamove kutoka juu kushuka chini nakama supply na demand wako na nguvu sawa basi soko linakua liko katika usawa yani haliendi juu sana wala halishuki sana linakua liko kwenye consolidation.
Kwahiyo wakati demand wananguvu ndio hapa huwa tunabuy na wakati hawa supply wananguvu basi hapa huwa tunasell na pindi supply na demand wakiwa na nguvu sawa hapa huwa tunasubiri maana hatujui wapi soko litaelekea.
Sasa basi ili utambue wapi demand wataanzia na kumalizia na pia ujue wapi supply wataanzia na kumalizia ni lazima utumie support na resistance zones na kwa maelezo haya hapa ndipo tunapata jibu kumbe support na resistance ni zone muhimu ambazo zinatufanya tutambue force ya soko iko vipi.
Kama nlivyosema awali tunabuy kwenye support na kusell kwenye resistance ila je wapi support ilipo na wapi resistance ilipo? Tukasema support iko chini ni mfano wa sakafu na resistance iko juu ni mfano wa paa la nyumba, je ntawezaje sasa kujua hapa ndio niweke support na hapa ndio niweke resistance katika chart yangu? Hili ndio swali ambalo tutaenda kulijadili hapo chini na kabla hayujafika huko kwanza nataka tuangalie movement ya soko huwa iko vipi then tutarudi kwenye sehemu gani yapaswa niweke support na wapi niweke resistance.
Kama tulivyosema awali soko linatembea up au down kutokana na force mbili za demand na supply na kuna wakati pia huwa linatulia sehemu moja.
Kwahiyo kutokana na maelezo hayo basi soko linatrend za aina mbili kuu na moja ni hiyo ya consolidation.
Tuko na uptrend na downtrend
Ambayo uptrend inatokea kipindi demand au buyer wanapokua na nguvu kuliko supply au seller… Na downtrend hutokea kipindi ambacho hao supply au seller wanapokua na nguvu kuliko demand au buyer na pia endapo wote watakua na nguvu sawa basi hapo tunasema soko liko kwenye consolidation.
Sasa hizi trend ndio nataka tuanze nazo kwanza huwa zinakua kua vipi kabla hatujaenda kwenye support na resistance tena
SUPPORT na RESISTANCE ni nini hasa?
Support na resistance ni zone muhimu sana ambazo zinatufanya tutambue demand na supply walipo.
SUPPORT
Support ni kama sakafu katika nyumba yako au chumba chako na hapa ndio hasa buyer huwa wanapatikana kusubiri price ifike wao waichukue na kuipeleka juu zaidi, kwahiyo hapa kwenye support ndio sehemu ambayo huwa tunabuy endapo price itakua imefika hapa na ikawa imekidhi vigezo vyote.
RESISTANCE
Hii ni kama sling board ya nyumba au chumba chako, ukisimama hapo kwenye sakafu yani kwenye support na ukiangalia juu ya paa la nyumba au chumba unaangalia kwenye resistance. Why support ni kama sakafu na resistance ni kama paa la nyuma?
Embu fikiria endapo ungekua umejenga nyumba isiyo na paa then ukasimama ndani ya nyumba na kuangalia juu, hivi macho yako yangekua na ukomo wakuangalia? Obvious hapana coz ungeangali pasipo kikomo but uwepo wa paa la nyumba linafanya ukiangalia juu macho yako yanagonga juu ya paa na kuishia hapo….na hata kwenye support endapo ungekua umejenga nyumba hewani then huku weka sakafu au ghorofa ya juu isiwekwe sakafu then uambiwe usimame unadhani nini kitatokea? Obvious utaanguka hadi ukutane na support itakayokufanya au kukuzuia usiendelee kudrop na hivi ndivyo ilivyo kwa price ikipita sehemu ambayo hamna support huwa inatembea coz sehemu isiyo na support huwa hamna force pingamizi ambayo ni demand force ambayo itazuia price isidondoke ila ikifika kwenye support itatulia maana itakua imekutana na force zuizi na ndivyo ilivyo pia kwenye resistance.
Sasa basi baada ya utangulizi huu wa awali nadhani sasa ni wakati wa kuingia kwenye kuzijua kiundani hizi zone za support na resistance vile zinavyofanya kazi na jinsi ya kuzitambua.
Soko linapokua lipo kwenye uptrend huwa haliendi moja kwa moja kama mstari mnyoofu ambao umepigwa na rula hapana huwa linakwenda na kutengeneza mikunjo flani flani kila baada ya muda na hiyo mikunjo huwa tunasema soko limefanya correction au retracement na utaijuaje retracement kwenye uptrend?
Utaijua pindi soko linapomove kwenda juu na ikafikia mahali likaanza kurudi chini kidogo then ghafla linaanza tena kuelekea juu…basi hapo huwa ndio tunasema trend ipo kwenye retracement au ipo kwenye correction.
Na pia kwenye downtrend huwa inatokea kwenye supply zone kuja chini so nayo huwa haiji kama mstari mnyoofu inakuja chini na kutengeneza correction au retracement ambapo humu kwenye downtrend tunategemea kuona wakati price inashuka basi kunakua na mikunjo inayoelekea juu kidogo then price inaendelea tena katika uelekeo wake na hapa ndio tunasema kwamba trend imeretrace au imefanya correction.
Na katika consolidation huwa inatokea wakati soko liko kwenye usawa yani haliendi juu sana wala haliendi chini sana…kama likienda juu hatua mbili basi litarudi chini hatua mbili pia so hapa ndio tunasema ipo kwenye usawa.
Ngoja tuone mifano sasa ya hizo trend kabla hatujaenda mbele zaidi
Na hii nayo ndio downtrend mikunjo ndio kama unavyoiona hapo na hiyo mikunjo ndio ya correction au retracement tulisema
Sasa basi baada ya kuonesha hizo trend kwa mifano michache utaona kwenye uptrend huwa inatengeneza higher high na higher low yani wakati price inapanda juu ikianza kutengeneza correction itapinda na kutengeneza kama pembe tatu hivi kwajuu hiyo ndio tunaita higher high(HH) na pia ikishashuka hadi level flani lazima itarudi kuelekea na uptrend yake na wakati itakapo rudi itatengeneza tena mkunjo kwa chini na hiyo ndio tunaita higher low kwamaana kwamba ilikua iko higher coz inaelekea juu ila ikashuka kutengeneza correction chini yani low ndio tunasema higher low
Na kwenye downtrend nayo huwa hivyo hivyo wakati inashuka lazima ifanye correction coz haiwezi kwenda kama mstari mnyoofu na ikifanya correction kwakua yenyewe ni downtrend yani inaelekea chini basi kwenye correction tutaona inapanda kidogo na wakati inapanda itaenda kidogo then itaweka mkunjo kama wa pembe tatu kwamaana itarudi tena chini ili kuendelea na trend yake basi ule mkunjo wa juu tutauita lower high kwamaana ilikua inaelekea chini coz ni downtrend but ikapanda juu kidogo nakutengeneza mkunjo juu kidogo yani high na ndio maana tukasema lower high na pia ule mkunjo wa chini yake huwa tunauita lower low yani uelekeo ni chini na mkunjo imetokea chini pia
Na hivyo ndivyo ilivyo sasa kwenye hizo trend nlikua nataka tuzione hizo trend na hiyo mikunjo yake ambayo hiyo mikunjo ndio hasa huwa tunaitumiaga kutafutia zone za support na resistance, kivipi? Tutaona si muda kwa sasa naomba urudie kuangalia hizo trend na pia uielewe hiyo mikunjo ya higher high, higher low kwa uptrend na lower high, lower low kwa downtrend.
Kwa kawaida katika market huwa price inakwenda juu na inashuka chini na kuna wakati huwa inatulia sehemu moja na sasa basi swali limakuja je ni nini huwa kinasababisha market iwe katika mtindo huu?
Na hili ndio swali ambalo linatakiwa lijibiwe na traders wote wa forex coz kwakujibu hili swali basi litafanya ujue nini chakufanya kwenye market, yani utrade muda gani na pair gani na muda gani usitrade.
Najua jibu unalijua ila wacha na Mimi nijibu na kuongeza idea au kama haujui basi ntakua nimekusaidia katika safari yako ya forex, kumbuka forex ni yakila mmoja coz forex sio kipaji sema mtu anazaliwa nacho hapana, bali forex ni ujuzi ambao mtu anaupata kwa mafunzo endapo anapenda so kwakua uko hapa naamini unapenda na ndio maana kila nkijuacho nakiweka hapa ili wote twende sawa.
Sasa ngoja tuone jibu la swali letu hapa chini.
Katika forex huwa kuna kitu kinaitwa pair na kingine kinaitwa currency hili najua unalifahamu na kama haulifahamu basi usijali utafahamu hapa
Pair ni muunganiko wa currency mbili na mfano wa pair ni EURUSD, NZDJPY, GBPCAD na kadhalika, na pia mfano wa currency ni EUR, USD, JPY, CAD, GBP, NZD na kadhalika.
Kwahiyo pair haiwezi kukamilika bila currency mbili kuungana hili muhimu unatakiwa uelewe.
Pia katika forex huwa hatutrade currency bali tunatrade pair so hata kwenye kufanya uchambuzi yani analysis huwa tunafanya kwenye pair ili hili ni kosa kubwa and why kosa kubwa, ntakuonesha hapa.
Mara nyingi tunabuy kama trend ikiwa up na tunasell kama trend ikiwa down na ikiwa kwenye consolidation huwa tunatulia coz hatujui soko litaelekea wapi zaidi, ingawa kuna baadhi ya consolidation huwa zinatradika kwa maana zinakuaga na pips hata 10 mbaka 15 so unaweza ukawa unatrade zone tu zone yani kutoka kwenye support hadi kwenye resistance na kwenye resistance to support, tutaona hapo baadae kwa kadri tunavyoendelea na somo letu la support na resistance ambalo ndio tunaendelea nalo.
Sasa basi ili soko liende juu yani uptrend basi lazima kwenye pair kuwe na currency ambayo ni weak na nyingine strong na ile strong ndio inaipeleka price juu…mfano ukiwa na pair ya EURUSD ukaona inapanda juu inamana hapa EUR ni strong na USD ni weak so ndio maana EUR ameweza kucontrol price au movement ya pair.
Na ukiona soko linamove kwenye downtrend basi ujue hapo katika pair kuna currency moja ni dhaifu na nyingine inanguvu, mfano USDJPY ukaona inamove down hapa jua kabisa USD ni dhaifu na JPY inanguvu ndio maana hii pair inamove kuelekea juu, kuna mtu hapa namuona hajanielewangoja nirudi hapa kwanza ili tuende sawa.
Katika pair kuna currency mbili na hizo currency kuna ambayo inaanza na kuna ambayo inafuata ukihesabu kutoka kushoto kwenda kulia, kwamfano EURUSD hii ni pair ambapo EUR ndio imeanza mwanzo na USD ndio imefuata na pair zote huwa tunahesabu hivi, sasa basi ili price iende juu basi lazima huyu anaeanza awe na nguvu kumpita anaemfuata so kwa hiyo pair ili iende juu basi ni lazima EUR awe na nguvu kumpita USD na ili market ishuke chini basi lazima EUR awe dhaifu kumpita USD so inamaana kwamba USD anatakiwa awe na nguvu kumpita EUR ndio aweze kupeleka price chini, tumeelewana sasa hapa
Kwahiyo popote unapoona soko linamove kutoka juu kuja chini yani kutoka kwenye resistance kuja kwenye support basi hapo currency ya pili ndio inanguvu kuliko currency yakwanza na ukiona inamove kutoka kwenye support kwenda kwenye resistance basi hapo jua currency ya kwanza inanguvu kuliko currency ya pili, simple like tha
Kitu cha msingi ambacho watu wengi huwa hawakifanyi katika analysis zao kutenga pair katika currency zake mbili then ndio uanze kufanya analysis.
Kabla hujafanya analysis zako kwa pair Fulani hakikisha kwanza unaitenga katika mafungu mawili na hii ni kwasababu pair ni muunganiko wa currency mbili na ili soko liende juu au chini lazima currency moja iwe na nguvu na nyingine iwe dhaifu na sio pair yote ndio inauwezo wakupeleka price juu au chini, no, bali ni currency, hii iweke kwenye ubongo wako.
Sasa ukishaigawa katika mafungu mawili basi sasa ndio tunaanza kufanya analysis kwenye currency moja moja, tutaanza na yakushoto then tunakuja yakulia….ngoja tuone mfano hapa venye tunatakiwa tufanye.
Kwamfano unataka utrade pair ya USDCHF basi tutaigawa katika mafungu mawili ambayo ni USD na CHF then hatua inayofuata tutaanza kuanalyz USD, sasa utaanalys vipi USD basi hapa ndipo tunapochukua pair zote zenye USD tunazichambua tuone je USD katika pair hizo zingine ameweza kuipeleka trend juu au hakufanikiwa ila amefanikiwa kuipeleka chini, basi kama atakua kaipeleka juu kwa pair zake zote na tukaona ananguvu basi tunanote pembeni then tunakuja kwenye currency ya pili ambayo ni CHF nae tutamfanyia analysis kwenye pair zake zote ambazo yeye yumo tutaangalia kama ananguvu au hana nguvu au yupo katikati yani hana nguvu sana wala hayuko dhaifu sana na ili ujue kwamba yupo katikati basi utakuta pair zake nyingi ulizozichambua price ipo kwenye consolidation, so nayo utainote kwenye daftari lako la uchambuzi.
Baada ya hapo sasa utakuja kuangalia zile pair ambazo USD na CHF wanachangia currency, kwamfano USDJPY na CHFJPY au EURCHF na EURUSD na zingine nyingi, kwenye hizo pair wewe utaangalia hivi.
Kwenye USDJPY utaangalia je USD ananguvu na amefanikiwa kuipeleka price juu, kama ndio basi utajua USD ananguvu kuliko JPY unaweka jibu pembeni, then unakuja kwenye CHFJPY utaangalia je CHF ananguvu na amefanikiwa kuipeleka price juu Au hapana, kama jibu hapana basi utajua hapa JPY alikua na nguvu kuliko CHF kwahiyo utaandika jibu lako.
Na baada ya kumalizia hapo basi utasema hivi kama USD ananguvu kuliko JPY na JPY ananguvu kuliko CHF je kati ya USD na CHF nani atakua na nguvu kuliko mwenzie, umepatia jibu ni USD so katika pair yetu ya USDCHF basi tutaenda kubuy coz price itakwenda juu na hapa tunasema USD ameicontrol price.
Na kama ungekuta CHF nae ananguvu kuliko JPY basi basi hapa inabidi uache kwanza au ntakwambia ufanye nini hapa chini ila kwa Leo ngoja tuishie hapa kwanza and fanyia mazoezi.
kuna wakati unaweza ukawa unafanya analysis zako za pair ya USDCHF ndio ilikua reference pair yetu hii…so unaweza ukafuata process zakuichambua hii pair na ukatumia reference mbali mbali na ukagundua pair zote zinanguvu na tulitumia reference ya USDJPY na CHFJPY ambapo kwenye USDJPY ukakuta USD ananguvu kuliko JPY na kwenye CHFJPY ukakuta CHF ananguvu kuliko JPY pia, hapa nkasema unatakiwa uachane na USDCHF coz unakua hujui nani anaicontrol price labda kama unascalp unaweza ukatrade but kumbuka hizi currency za USD na CHF wanashare currency nyingi pia kwenye pair zao, na nlitoa nyingine ya EURCHF na EURUSD so kama kule ulipata jibu lenye mkanganyiko basi unarudi na kwenye hizo pair nazo unaanza kuangalia kati ya USD na CHF nani atakua na nguvu kuliko mwenzie.
Kwenye EURUSD ukishaichambua na ukagundua EUR ananguvu kuliko USD yani ukiona price inapanda juu basi unanote pembeni, then unakuja kwenye EURCHF naukikuta kwenye hii pair CHF ndio ananguvu kuliko EUR yani price inashuka chini yani tunasell hapa napo unanote jibu lako pembeni, then unarudi kwenye pair yako ya USDCHF lazima utakuta inadrop coz CHF atakua na nguvu kuliko USD na hii imetokana na uwezo wake wa yeye kuwa mkubwa kuliko EUR na wakati huo EUR ananguvu kuliko USD.
Pia ukienda kwenye pair kama EURJPY utakuta nayo inapanda juu unajua why, coz USD alikua na nguvu kuliko JPY na wakati huo EUR ananguvu kuliko USD so obvious EURJPY itakua inakwenda juu tena kwa pips nyingi tu.
Pia CHFJPY itakua inakwenda juu kwa kasi maana CHF atakua na nguvu hapo kama tulivoona kwenye analysis zetu hapo juu.
Na hii hali ndio huwa tunasema correlation of pair so ukishajua hii huna haja yakuomba zile chart ambazo wameandika pair nyingi za kuonesha correlation na uanze kuzikariri no, just do your analysis and utabaini kitu na kumbuka kwa kutumia njia hii unaweza ukafanya analysis ya pair moja na ikakupa muelekeo wa pair nyingine nyingi tu…so nenda kajaribu sasa
Kwa kawaida katika forex huwa tunacurrency 8 ambazo hizi ndio major currency, ambazo ni EUR, USD, GBP, JPY, CAD, AUD, NZD na CHF.
Hizo ndio currency ambazo zipo kwenye forex sasa…..na hizo currency tukiziunganisha ili tupate pair tunapata pair 28 na hizi ndio hasa zipo kwenye forex na kila mtu anazijua ila kwa mfano tu ni hizi hapa.
EURUSD
EURJPY
EURGBP
EARNZD
EURCAD
EURAUD
EURCHF
USDJPY
USDCAD
USDCHF
GBPUSD
GBPCAD
GBPAUD
GBPJPY
GBPNZD
GBPCHF
NZDUSD
NZDCAD
NZDAUD
NZDCHF
NZDJPY
CADAUD
CADJPY
CADCHF
AUDCAD
AUDUSD
AUDCHF
Hizo ni mifano tu ya pair so zingine utamalizia hapo ila mi nimetoa mifano tu hapo so hizo ndio pair kimsingi zinatakiwa ziwe 28 ila mi nimeandika kwa uchache tu ili kukufanya uzielewe.
Sasa tunapofanya analysis hapo kwamfano tunatrade pair ya EURUSD, tunachotakiwa kufanya ni kuitenga katika currency mbili ambazo zimeunda hiyo pair ambazo ni EUR na USD…na baada ya hapo sasa unaanza kuzichambua hizo pair zote ambazo EUR yupo unaangalia trend yake na uwezo wake na hizo pair zingine kama uko juu au chini ili ikufanye uelewe kama EUR anaonekana ananguvu au hana nguvu, kumbuka currency huwezi ukaifanyia analysis kwakuchora ila tunafanyia analysis pair maana kwenye platform za forex hakuna mahali utakuta USD iko pekeake wala ukakuta EUR iko pekeake ila utakuta muunganiko wa currency mbili ambazo zinafanya piar kwamfano hiyo EURUSD, so hilo unatakiwa ulijue kwanza.
So hapo ukishaangalia hizo pair zote za EUR najua utagundua kama EUR ni bearish kwakua pair zote alizopo anashindwa kupeleka price juu au bullish coz kwenye pair zote alizoko amefanikiwa kupeleka price juu.
Ukishamaliza hapo inabidi urudi kwa upande wa USD nae unamfanyia hivyo hivyo ili uelewe yuko bullish au bearish kwenye pair zake ambazo yupo na ukishamaliza hapo inabidi sasa ujiridhishe maana unaweza ukakuta majibu ambayo yanafanana, kwamfano ukikuta EUR anaonekana kwenye pair zake zote ni bullish na pia ukakuta USD nayo ni bullish hapo utashindwa kujua ukafanyeje kwenye EURUSD, so inabidi uchuchue reference pair kwamfano EURJPY na USDJPY angalia hapo kwenye currency ya JPY EUR alikua bullish au bearish ukiona ni bullish basi rudi kwa USDJPY nae ukiona ni bullish basi hiyo pair ya EURUSD inauwezekano wa kuwa kwenye consolidation coz USD na EUR wote wananguvu sawa hapo kaa pembeni ya market acha tamaa.
Na ukiona mmoja kati yao ni bullish na mwingine ni bearish basi hapo kuna ela …kwamfano ukakuta EUR ameweza kuwa bullish kwa JPY lakini USD amekuwa bearish kwa JPY basi hapo moja kwa moja tutabuy maana EUR ananguvu kuliko dollar coz EUR ameweza kuwa bullish kwa JPY na USD ameshindwa so hatoweza kupambana na EUR kama ameshindwa kwa JPY
Kama tulivyosema support ni mfano wa sakafu na resistance ni mfano wa Dari kwenye nyumba, sakafu inakusaidia uweze kusimama usiporomoke na Dari inakusaidia usiangalie mbali zaidi….
Ndivyo ilivyo kwenye market price ikifika kwenye support huwa inaishia hapo na kugeuza kurudi tena juu na ikifika kwenye resistance inaishia hapo na kugeuza kurudi chini ila hii inategemea na nguvu ya currency husika, kwamfano ukichukua pair ya EURUSD kutrade ukiona inatoka chini na kwenda juu na ikafika mahali ikageuza na kurudi chini basi hapo ilipogeuzia tunasema ni kwenye zone ya wanunuzi yani ndipo ilipo resistance na ikiwa inashuka chini ikafika mahali ikageuza basi hapo ndipo kwenye zone ya buyer na tunaita support so ndipo tutakapoweka mistari yetu juu ya resistance na chini ya support.
Ngoja tuone hapa chini venye tunachora hiyo mistari ya support na resistance sasa.
Hii mistari ya support na resistance huwa inakuaga na sheria zake rahisi sana pindi tunapozichora.
1 kwanza ni lazima ugundue mikunjo ya juu na chini, mikunjo ya juu ni resistance na mikunjo ya chini ni support.
2 weka mstari kwenye hiyo mikunjo ya juu ambayo tutaita resistance na weka mstari kwenye mikunjo ya chini ni support.
3 hakikisha mstari wa juu unagusa kwenye candlestick zaidi ya moja, yani kuanzia mbili na kuendelea na hata mstari wa chini pia ni lazima uguse kwenye candlestick zaidi ya moja kuanzia mbili na kuendelea.
4 kama mstari wa juu utagusa candle moja na wa chini pia basi hapo tutasema resistance na support haziko valid.
Ukishachora hiyo mistari ya support na resistance na ukahakikisha iko valid basi hapo ndio setup yako itakua imekamilika now unasubiri entry point ifike ili uingie sokoni.
Sasa basi katika support na resistance entry point zetu huwa tunasubiri price iende juu ikagonge kwenye hiyo line ya resistance then igeuze ianze kurudi chini kwa kuuza na kwenye support pia hivyo hivyo tu nasubiri price igonge line ya chini na ianze kurudi juu ndipo hapo tunakaa tayari kwa kununua.
Kitu muhimu ambacho unatakiwa ufanye wakati unataka kuingia sokoni kwakutumia support na resistance ni kwamba, wakati price ipo kwenye support ikagonga na kugeuza kurudi juu, unahesabu candle ya kwanza na yapili then ya tatu ikianza unaingia hapo ndio uhakika kwamba kweli price inapanda juu, na hata kwenye resistance pia unatakiwa usubiri hivyo hivyo yani ya kwanza na yapili ikianza ya tatu tu unaingia sokoni…ila kuna wakati mwingine huwa kunakuaga na candle kubwa sana ambayo inanguvu kwenye upande wa support ikiisha hiyo candle basi hainaaja ya kusubiri hadi zifike tatu coz kama ikitokea kwenye support inamaanisha kunastrong bullish movement so ni kubuy tu baada ya hiyo candle kuisha hadi kwenye resistance na ikitokea kwenye resistance basi ni kusell hadi kwa support.
Pia ukishaingia sokoni basi ni lazima ujihami maana forex sio science kuna wakati unaweza ukabuy katika sehemu sahihi ila ghafla soko likageuka na kurudi nyuma na kuendelea na safari yake ya awali, hii huwa inatokea sana na ndio maana huwa tunashauriwa kutumia stop los ambayo hii itatufanya tuwe salama zaidi hata kama soko likirudi nyuma litaishia kwenye SL yetu na kutuacha na ela zetu za mtaji bado zipo.
So katika support na resistance huwa tunaweka SL yani stop los nyuma ya mstari wa support na resistance, kwamfano kwenye support SL yake huwa tunaweka chini zaidi ya mstari wenyewe wa support na kwenye resistance huwa tunaweka juu zaidi ya mstari wenyewe wa resistance
Baada ya kuingia sokoni sasa ni lazima ujue wapi utachukulia faida yako, na Mara nyingi huwa inasisitizwa usiingie sokoni bila kujua wapi utaenda kuchukulia faida yako, maana hii itakufanya ushindwe kuelewa wapi utaweka TP yako yani take profit yako….na ukishindwa kuelewa wapi utachukua faida basi unaweza ukashangaa unachukua kijifaida hata chmwingine. natania asee…
Ila ukweli ni kwamba trader ni lazima ajue entry point yake na SL yake wapi ataweka pia ni lazima ajue TP yake wapi anaenda kuiweka na hii itamrahisishia hata yeye kucalculate pips ambazo atakwenda kuchukua kwa kila trade atakayoingia na pia itamrahisishia ajue anatakiwa aingie trade ngapi kwa siku ili afikie idadi ya pips anazo zihitaji.
Na kwenye support na resistance TP huwa tunaweka chini ya resistance na juu ya support, kwa maana kwamba kwenye support baada ya mstari wa support juu yake tunaweka TP na kwenye resistance baada ya mstari wa resistance basi chini yake hapo tuna weka TP… Na hii ndio tunaita zone to zone, yani unatoka ukanda mmoja na unaenda kuchukulia faida ukanda mwingine.
wakati resistance inabadilika kuwa support na support kuwa resistance.
Hii inatokea kipindi ambacho currency moja kwenye pair inakua na nguvu sana kuliko nyingine, so inaelekea ishindwe kuzuia isiingiliwe kwenye maeneo yake ya kujidai…ni kama team mbili za mpira moja ikiwa na uwezo sana na nyingine ikiwa haina uwezo sana mwenye uwezo sana ni rahisi kufika golini kwa asiye na uwezo na kufunga magori kiurahisi basi ndivyo ilivyo kwenye hizi pair kuna wakati currency shindani huwa zinakua zinauwiano usio sawa yani moja inakua na nguvu sana kuliko nyingine na hii hupelekea yenye nguvu kupita kwenye zone ya currency dhaifu bila kipingamizi na hapa ndipo breakout hutokea na breakout ikitokea kwenye support basi support inabadilika kuwa resistance na ikitokea kwenye resistance basi inabadilika kuwa support..
Kiurahisi chukulia mfano mtu akitoboa paa na akaenda hadi juu ya bati la nyumba akatua pale, bati ndio litakua support yake maana limemfanya asimame pale wakati mwanzo kabla hajatoboa bati lilikua ni resistance yake maana ndipo alipokua anaangalia wakati aliposimama kwenye sakafu…na ndivyo ilivyo hata kwenye price inapovunja resistance na kuingia upande wa pili huwa tunaichukulia ndio support maana imefanya price ianzia hapo na kinyume chake kwenye support nayo ikivunjwa ndio inakua resistance.