Kutokana na ongezeko la watumiaji wa Safaricom M-Pesa wanaohitaji kutuma pesa kwenda Vodacom M-Pesa Tanzania, nimeamua kuandika makala hii ili kuwasaidia wale ambao hawafahamu jinsi ya kufanya muamala huo.
Fuata mtiririko ufuatao kufahamu jinsi ya kutuma pesa kutoka M-Pesa Kenya kwenda M-Pesa Tanzania
- Kwenye simu yako, fungua application ya ku manage SIM CARD (Sim Toolkit)
- Chagua Safaricom kisha fungua M-Pesa
- Chagua “LIPA NA MPESA”
- Chagua Pay Bill kisha weka namba ya biashara yaani Business Number ambayo ni 255255
- Sehemu ya kuweka “Account Number” weka namba ya simu ya Tanzania kwa kuanza na code ya Tanzania pekee bila + yaani 2557XXXXXXXX
- Andika kiwango unachotaka kutuma katika Kenyan Shillings KES.
- Ingiza namba yako ya siri ya M-Pesa halafu kubali muamala.
Baada ya kukamilisha mtiririko huo, utaulizwa kama unataka kuzuia muamala, uandike herufi yoyote ndani ya sekunde 25, usiandike chochote, acha kama palivyo au waweza bofya CANCEL, baada ya hapo utaambiwa “Thanks for using M-Pesa” na kiwango ulichotuma kitatumwa moja kwa moja kwenye namba uliyotuma Tanzania.
NJIA MBADALA
Iwapo upo Tanzania, na ungependa kutoa pesa moja kwa moja kutoka kwenye laini yako ya Safaricom bila kuituma Vodacom kwanza, unachopaswa kufanya ni ku bofya namba ya M-Pesa ya Safaricom ambayo ni *840#.
Kama ndio mara yako ya kwanza kubofya namba hiyo, utaambiwa uandike eneo ulilopo, utaandika eneo lolote ulilopo kwa Mfano, Dodoma, au Arusha.
Baada ya kufanikiwa kuhifadhi eneo ulikopo, utabofya tena *840# na utachagua ROAMING PICK UP, hapo sasa utaweka nambaya wakala wa M-Pesa unapotaka kuchukua pesa yako na utaendelea kufuata maelekezo kama kawaida, kwenye njia hii ya pili, badala ya kuweka kiwango kwenye Shilingi za Kenya, unaweka katika Shilingi za Tanzania.
Endelea kuwa pamoja nasi kufurahia elimu tunayoitoa kupitia blog hii ya Biashara ya Forex.
Habari yako samahani naomba kuuliza mtoto wangu anataka kunitumia pesa kutoka kenya anashindwa kutuma naomba msaada wa maelekezo ili nimwambie anitumie