Makala hii itaenda kukuelimisha jinsi ya kutumia program ya Metatrader 4 au kwa kifupi mt4 kukuwezesha kufanya biashara ya Forex.
Metatrader ni program maalum inayotumika kuwezesha ufanyaji wa biashara ya Forex yaani kufungua position, pamoja na kukupatia chart ambazo zitakuwezesha kuona uelekeo au historia ya pair za Forex na pia kukuwezesha kufanya uchambuzi wa pair hizo kwa kitaalam technical analysis.
Kuanza kutumia program hii, yakupasa uwe na account katika moja ya broker utakayemtumia ku trade Forex.
Metatrader ina version kuu mbili, Metatrader 4 na Metatrader 5, hizi ni programu mbili tofauti na haimaanishi kwamba Metatrader 5 ni toleo la juu la metatrader 4, la hasha. Hizi ni program tofauti kabisa, ingawa zinatengenezwa na kampuni moja, na programu ambayo inatumika zaidi kwa biashara ya Forex, ni Metatrader 4 au kwa kifupi MT4.
Jinsi ya ku-install Metatrader4
Program ya Metatrader 4 inapatikana katika vifaa vyote tunavyotumia ku trade Forex yaani simu, PC pamoja na Mac. Zipo version za mt4 za Android, iOS na hata Windows kwa ajili ya computer yako.
Kuweza kutumia vyema program hii ya Metatrader 4, yakupasa uwe umeshafungua account kwa broker unayemtumia.
Ukishatengeneza account, aidha kwa kutumia simu yako ya mkononi au kwa kutumia computer yako, fungua menu, au angalia menu iliyopo upande wa kushoto, utaona menu imeandikwa Downloads, bofya sehemu hiyo kisha bofya sehemu iliyoandikwa Platforms na utaona maelekezo pamoja na orodha za platform ambazo unatumia ili u download program hii ya Metatrader 4. Kama unatumia windows computer, bofya sehemu iliyoandikwa TemplerFX trader on windows, na kama unatumia simu ya mkononi, nenda moja kwa moja kwenye PlayStore kama unatumia Android, au AppStore kama unatumia iPhone au iPad, kisha search neno MT4 au neno Metatrader4 ambapo utaona program hii, na utai install.
Ukisha install, utaona option ya kufungua Demo account, ambapo una uhuru wa kufungua default demo account kutoka kwa watengenezaji wa program ya mt4, au waweza ingiza taarifa za demo account za broker wako.
Kama hutapenda kuweka demo account, una uhuru wa kuweka login na password zako za account yako uliyotengeneza kwa broker wako.
Kumbuka kwamba, taarifa zako za ku login, zipo kwenye site ya broker wako, kama unatumia broker wa templerfx, basi kupata taarifa zote, login kwenye site ya templerfx, halafu kwenye menu kuu, bofya sehemu iliyoandikwa Open an Account halafu chini yake, bofya new account. Kwenye orodha ya account za kutengeneza, utaulizwa uchague aina ya account ya kutengeneza, chagua yoyote inayokufaa kati ya either DEMO ACCOUNT (kama hupo tayari kuanza na real account) au chagua LIVE UNIVERSAL FX kutengeneza live/real forex account.
Mara baada ya kutengeneza, utapewa Login Id, na Password. Ambazo sasa, ndio unazopaswa kuzitumia ku login kwenye program yako ya Metatrader 4.
Endelea kuwa nasi katika makala hii ambayo itaendelea kukufundisha jinsi ya kutumia menu mbali mbali zilizopo kwenye program uliyo install ya Metatrader 4.
Napenda kukufahamisha tena, kama huna account bado, bofya link ifuatayo kutengeneza account yako ya Forex.
Kama una maoni, ushauri, au swali, usiache kutushirikisha kwa kuandika kwenye sehemu ya comments, au kuwasiliana nasi kwa kubofya menu ya Telegram hapo juu.