Karibu tena tuendelee kupeana elimu kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo biashara ya Forex. Leo tutaenda kuangalia jinsi ya kuweka na kufunga order kwa kutumia programu ya Meta Trader 4 au kwa kifupi MT4 kama ilivyozoeleka.
Kama ambavyo tulisoma kwenye makala ihusuyo jinsi ya kutumia MT4 inayopatikana >> HAPA << leo tutajifunza juu ya namna ya kuweka na kufunga order za forex kwenye programu hii ya MT4. MT4, ni programu maalumu iliyotengenezwa kukuwezesha kuweka order (position) za forex, pamoja na kuwa na chart mbali mbali ambazo zinaonesha historia ya pair fulani ya Forex kwa nyakati zilizopita, ambapo historia hiyo, inaweza kukusaidia kufanya uchambuzi juu ya uelekeo wa pair husika.
Programu hii ya MT4, inaweza kutumiaka kwenye simu yako ya mkononi, au kwenye computer yako, kuipata programu hii kwenye simu yako ya mkononi, iwapo unatumia simu zenye mfumo wa Android, nenda kwenye PLAY STORE na tafuta neno meta trader 4 au mt4, na utaiona, kisha install, na iwapo unatumia simu za iPhone, vivyo hivyo nenda kwenye App Store ya simu yako, kisha tafuta neno MT4 au Meta Trader 4, kisha install.
Iwapo unatumia computer, login kwenye account yako ya Forex kwa broker uliyejiunga naye, halafu nenda kwenye menu ya DOWNLOADS, kisha chagua version ya Meta Trader 4 inayoendana na computer unayotumia, yaani kama ni Windows, au kama ni Mac, baada ya hapo uta install kama unavyo install programu nyingine kwenye computer yako.
Kama bado huna account ya Forex, bofya link ifuatayo ili utengeneze account kwa broker tunayemtumia zaidi Africa Mashariki wa TEMPLER FX
BOFYA HAPA KUTENGENEZA ACCOUNT
Ukishafanikiwa ku install program ya MT4, sasa yafuatayo ni maelekezo ya jinsi ya kufungua na kufunga order (au position)
Kufunga na kufunga order kwa kutumia computer
Kwenye kufungua order, kuna vitendo vikuu viwili kwenye pair husika, ni aidha unanunua yaani BUY au unauza yaani SELL pair husika.
Kwenye ku BUY au ku SELL kuna order za aina kuu mbili ambazo ni INSTANT na ya pili ni PENDING:
- BUY or SELL kwa kutumia instant execution
- BUY or SELL kwa kutumia pending order
Hatua ya kwanza unapaswa kufanya, ni kufungua programu yako ya META TRADER 4, na ukiangalia kwenye menu iliyoko juu, utaona kitufe kimeandikwa NEW ORDER, bofya kitufe hicho kama inavyoonekana pichani, halafu utaona order za aina mbili either instant execution, ambayo ni order inayojazwa muda huo huo, au pending order ambayo ni order inayojazwa baada ya bei husika uliyoweka kufikiwa
Kabla hujabofya kutufe cha SELL au BUY, kuna sehemu za kuangalia, nazo ni kama zifuatazo:
Symbol, hii ni PAIR ambayo unatarajia ku deal nayo either kwa ku SELL au kwa ku BUY
ya pili ni Volume volume au ujazo kwa jina lingine inaitwa LOT SIZE, hiki ni kiwango ambacho unakitumia kulingana na mtaji ulio nao, kwa mfano kama unaanza kwa mtaji mdogo, unashauriwa kuweka volume ya chini kabisa, ambayo ni 0.01. na utakuwa unaiongeza kulingana na jinsi mtaji wako unavyokua.
Kingine cha muhimu ni Stop Loss pamoja na Take Profit, stop loss au SL, ni kiwango unachotarajia kukiweka, kwamba iwapo pair imeenda kinyume na matarajio yako, basi utakua tayari kupoteza kiwango flani kwa kuamua kuweka stop loss.
Ya tatu ndio sehemu ya kuchagua kama ni Instant Execution au ni Pending order.
Ukishajiridhisha na taarifa ulizo jaza, uta bofya button ya BUY au SELL kulingana na jinsi unavyo predict uelekeo wa soko kwa pair uliyoamua ku deal nayo.
Mara baada ya kubofya SELL au BUY, ikishakua executed, utaona order yako ikiwa inaendelea either kukua, iwapo ulienda uelekeo sahihi, au ikiendelea kuwa ndogo iwapo ulienda uelekeo ambao sio, na uki right click kwenye order hiyo, una uwezo wa kuifunga kwa kubofya CLOSE
Makala ifuatayo, tutajifunza zaidi jinsi ya kutumia MT4 version ya simu.